Katika Makala ya Siha Njema tunaangazia Ripoti ya umoja wa mataifa , ya mwaka 2020 ya huduma za upangaji uzazi,mwaka moja tangu kuzuka janga la Corona .Ripoti hiyo imebaini kushuka kwa huduma hizo na kuonya mataifa mengi huenda ikapunguza uwekezaji wao kwenye huduma za kupanga uzazi kutokana na kuathirika kwa chumi zao .