Siha Njema

Utengano wa familia unaweza kuleta shinikizo la damu au kisukari


Listen Later

Wanadamu ni viumbe ambao hukamilika wanapokuwa kwenye jamii ambapo wanaweza kuelezea hisia zao,kujihisi wanathaminiwa na wana mchango kwa wengine. Mambo  hayo yanapokosa,inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya.Na hii ni hali ambao hukuwa nao wakimbizi ambao wametenganishwa na wapendwa wao.

Katika kambi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana,kaskazini mwa Nchi ya Wakenya,tulizungumza na wakimbizi ambao walilazimika kutengana na wapendwa wao kwa sababu ya migogoro ya kifamilia,ukoo na hata vita.

Ingawa wamepata makao katika kambi ya wakimbizi bado maisha yao hayajakamilika .

Wengi wameishi kwenye hali ya upweke,huzuni na kiwewe  na kupata matatizo ya kiafya yakiwemo matatizo ya afya ya akili.

Aidha kuna wale ambao wamepatwa na maradhi kama shinikizo la damu ,kisukari,ukosefu wa usingizi na chanzo ni matatizo ambayo wamekumbana nao katika kambi,ugumu wa maisha bila watu walio karibu nawe ambao unaweza kuzungumza nao na kuliwazana.

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC pamoja na shirika la msalaba mwekundu nchini ,KRC,katika kujaribu kukabili hali hiyo ,zinatekeleza mpango wa kujaribu kurejesha mawasiliano na uhusiano wa familia za wakimbizi.

Kwa kuwatafuta namna ambao wakimbizi hao wanaweza kuwasiliana kupitia ujumbe wa kuandikiwa au  kwa njia ya simu,mashirika hayo wanasema wamefanikiwa kuwarejeshea tabasamu wachache wenye bahati na wanaendelea kuwasaka wanafamilia zaidi kila mwaka.

Matunda ya mpango huo yameonekana miongoni mwa wakimbizi wanaozungumza na jamaa zao na pia kwa wahudumu wa kujitolea wanaotangamana karibu kila siku na wakimbizi hao kwenye kambi.

...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Siha NjemaBy RFI Kiswahili


More shows like Siha Njema

View all
Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners