Babananiii

FAIDA YA KAZI PT. 2


Listen Later

*FAIDA YA KAZI* Inaendelea....
*2. KAZI ITAKUONGEZEA FURAHA*
Licha ya uchumi kazi inaweza kuwa jambo la kufurahisha sana. Mtu hufurahia anapofanya kazi yenyewe, na hufurahia pia, anapoona matokeo ya kazi yake, hasa iwapo kazi hiyo iwe ni ile inayohusiana na kuleta mabadiliko mapya mbalimbali.
Isitoshe, shughuli za kazi zinasaidia sana kupitisha wakati na kumwondolea mtu mawazo yasiyofaa. Vile vile kazi huweza kuwa njia nzuri sana ya kumwezesha mtu akutane na watu wengi mbalimbali ambao humchangamsha kwa njia nyingi; na mara nyingi kazi imekuwa ndio njia muhimu ya kujipatia marafiki wa aina mbalimbali. Watu wengi waliokwishastaafu huanza kulalamika kwamba wanakosa kitu cha kuwashughulisha vya kutosha, na zaidi sana wanasumbuliwa na *upweke* unaowaandama kutokana na kuwakosa wale ambao walikuwa na mazoea ya kukutana kutana nao katika kazi.
*"Kweli mtu akikunyima kazi amekuondolea furaha katika maisha."*
*3. KAZI ITAKUFANYA MAISHA YAWE NA THAMANI*
Hatupo hapa duniani ili tule, tunywe tustarehe, na tuishi kwa kujifikiria nafasi zetu sisi wenyewe tu, bali maisha yetu yana lengo; *nalo ni kutumika kwa Utukufu wa Aliyetuumba.*
Watu ambao hawana lengo kama hilo mara nyingi maisha yao hujaa wasiwasi, tupu (vanity) na kutotosheka. Baadhi yao huwa ni wale ambao unawaona wakihangaika mchana na usiku kuwinda shibe na starehe. Baadhi ya wengine ni wale ambao unasikia kwamba wameamua kujiua wenyewe kwa vile hawaoni faida ya kuendelea kuishi.
Lakini ukiishi maisha yenye lengo la utumishi utatambua jinsi ulivyo na thamani kubwa kwa wengine, na hutathubutu kuzurura ovyo bila kazi yoyote japo uwe tajiri kiasi gani. Pia hutathubutu kukomesha maisha yako mwenyewe kwa vile utajiona kwamba wewe sio mali yako mwenyewe, bali upo kwa kutimiza lengo fulani. *"Watu wengi wanaotosheka katika maisha huwa ni wale ambao wakitazama nyuma wanaridhika kuona kwamba wametoa mchango wao katika kuleta maendeleo na ustawi wao na wa wenzao; na wakitazama mbele wanaona kwamba bado wanayo nafasi kubwa ya kuendelea kutimiza lengo kama hilo."*
Itaendelea kesho.........
Ahsanteni
...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

BabananiiiBy Fabian C. Mwakabanje