*JINSI YA KUWEKA MIPANGO*
A. Marlene Wilson anasema kwamba mchakato ulioratibiwa unapaswa kuzingatia kanuni zifuatazo:
1. *Malengo;* ni matokeo yanayotazamiwa; mahali ambapo mtu au taasisi inataka kufika -- hatima au maazimio yake.
2. *Maazimio;* kutafsiri malengo na madhumuni kwa njia iliyo wazi na rahisi ya kueleweka na kutekelezeka (wakati mwingine huitwa mipango kazi).
3. *Kazi;* ni mambo gani ya kuyatekeleza ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
4. *Mipango;* ni mbinu na mtiririko wa kazi ili kufikia malengo.
5. *Bajeti* ni sehemu ya mpango iliyoainishwa kitarakimu na kuwekewa kiasi cha fedha.
6. *Ratiba;* ni mpango wenye tarehe za utekelezaji na watumishi wahusika.
7. *Tathmini;* ni kuipima kazi inayofanyika kama vinawiana na mipango iliyowekwa. Kubaini iwapo mpango umefikia malengo yaliyokusudiwa.
B: Ili timu iwe na tija ni sharti mipango au kazi ifafanuliwe waziwazi - iandikwe.
1. Mungu ni Mungu anayekusudia na kutenda mambo yake (Isaya 46:11).
2. Mfano wa Wanawali kumi: watano waliojiandaa na watano wapumbavu (Mathayo 25:1-13)
3.Tunajifunza Daudi alivyoandaa mpango wa kulirejesha sanduku lakini uliokuwa kinyume na mpango wa Mungu (1 Nyakati 13:1-15:19; Kutoka 25:10-15)
JINSI YA KUANZISHA HUDUMA ZENYE TIJA (VIJANA)