Anaitwa DOLOMOI FRANCIS, kwa jina maarufu anafahamika kama DOLO. Ni moja ya waasisi wa kundi la Wachuja Nafaka na Wanaume TMK. Kutoka maeneo ya TEMEKE. Tumepata bahati ya kukaa naye mezani na ametupitisha kwenye safari yake ya muziki. Kuanzia akiwa hajawa Dolo, mpaka hivi sasa akiwa bado anapeperusha vyema bendera ya TMK.
#MezaniNaDolo #MezaHuru