Zipo nyakati ambazo kitu kigumu sana kufanya huwa ni kusema ukweli, au kunena lile ambalo Bwana Mungu amekupa kunena. Jambo hili huweza kuwa na matokeo hatari kwako hivyo kukufanya uogope kunena kama siyo kusema uongo kabisa. Lakini Biblia inasema usiogope kunena lila likupasalo hata kama itatishia kugharimu uhai wako. Nena, usiogope. Biblia inasema usiogope.