Maisha Ni Kuthubutu Podcast

Tabia Tano (05) Za Kuepuka Ili Utimize Malengo Yako.


Listen Later

Tabia Ina nafasi ya moja kwa moja ya wewe kutimiza au kutotimiza malengo yako, kwa bahati mbaya watu wengi wanachukulia poa sana suala la tabia.
Ukitazama elimu kuhusu tabia gani zinaleta mafanikio na kutimiza malengo yako kwa kishindo haitolewi kwa ukubwa zaidi katika mazingira ambayo tupo.
Unauliza “Innocent” ni kwa namna gani?
Swali zuri Mtaalamu.
Ni hivi....
Kuna tabia ambazo zilifanya utimize malengo yako ya mwaka 2022?
Kuna tabia ambazo zilifanya ushindwe kutimiza malengo yako ya mwaka 2022?
Vizuri, kwa kupata majibu na umeanza kuona tabia Ina nafasi kubwa ya kutimiza au kutotimiza malengo yako.
Kwa mifano;
Mfano wa kwanza. Je mtu ataweza kupungua uzito akiwa na tabia ya kula ovyo vyakula vya mafuta, Sukari na ana tabia ya kutofanya mazoezi?
Jibu ni hapana! Kumbe tabia hizi ni kikwazo.
Mfano wa pili: Mtu anataka kuwa na kiasi cha millioni moja mwisho wa mwaka na akawa kila mwisho Mwa mwezi kwenye akaunti anaweka laki moja kama akiba, Atafanikiwa kufika lengo Lake mwezi disemba.
Kumbe tabia ya kuweka akiba ni chachu ya kufikia lengo la kifedha si ndiyo mtaalamu?.
Lakini...
Leo utajua tabia gani za kuepuka ili utimize malengo yako, ukweli kuna tabia fulani fulani ambazo ukiziepuka ni suala la muda wewe kutimiza malengo yako, kama unajitihada.
Unataka kujua tabia gani uepuke si ndiyo?
Sekunde chache kutoka sasa utaenda kujua tabia hizi ndani ya podcast ya Maisha ni kuthubutu...
....maana huku umepewa kila kitu katika episode hii ambayo Ina dakika 19 tu za kufanya mwaka huu kuwa wako wa kutimiza malengo yako.
Cha kufanya ni rahisi.
Bofya link hapa chini sasahivi usikilize episode hii na utajutia kwanini hukusikiliza miezi sita iliyopita, hujachelewa Bofya hapa chini Mtaalamu upate madini.
...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Maisha Ni Kuthubutu PodcastBy Innocent Ngaoh