Uchumi na Biashara

Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ya mitumba


Listen Later

Katika podcast hii tunaangazia panda-shuka za wafanyabiashara wa nguo za mitumba wakati huu wa janga la korona.
Mmoja wa wafanyabiashara hao mjini Kitale kwa jina Andrew Chongo anayeuza suti za mitumba anasema kupigwa marufuku kwa uagizaji wa baadhi hizo kulisambaratisha biashara zao na hata wengine kulazimika kubadili biashara ili kuzikimu familia zao.
Chogo anasema amri ya Rais Kenyatta ya kuondoa kafyu itastawisha uchumi wa taifa hili ikizingatiwa kwamba sasa wanaweza kusafiri ama kuagiza nguo kutoka mataifa mengine.
Hata hivyo Chogo analipendekezea serikali kufufua na kuanzisha viwanda vya pamba na kuwawezesha wakulima kupanda mmea huo na kuwafuga kondoo aina ya merino ili kutoa ajira kwa vijana na kuwapiga jeki wakulima kiuchumi.
Mwanahabari wetu wa Trans Nzoia, Martin Ndiema amemhoji mfanyabiasha huyo.
...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Uchumi na BiasharaBy Standard Media