Sign up to save your podcasts
Or

UKILIMA WA MATUTA WAZALISHA CHAKULA - RUTH MASITA
Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi akina mama katika kijiji cha Mavirivirini kaunti ya Kwale wamekuja na mbinu za kukabiliana na athari hiyo kwa kutumia ukulima wa matuta kwenye harakati za kuhakikisha wanapata chakula cha kutosha. Itakumbukwa kwamba Kwenye kongamano kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi almaarufu COP 27 mwezi Novemba mwaka 2022 nchini Misri, rais wa Kenya William Ruto alisema serikali yake ina mzigo wa kuwasaidia wakenya milioni nne na chakula cha msaada hali inayolemaza miradi mingine ya maendeleo. Na kwenye mkutano huo viongozi wa mataifa na wataalamu waliafikiana kuwa ni sharti wabuni mbinu mpya na za kudumu zitakazokabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kama vile ubunifu wa mbinu mpya za kilimo. Na ni kutokana na wito kama huu ambapo baadhi ya kina mama wakulima kutoka kaunti ya Kwale wameanza kuzingatia mbinu mpya ya kilimo kwenye harakati ya kujinasua kutokana na kilimo cha kutegemea mvua nyingi ambayo ni nadra kwa sasa kutokana na kiangazi cha mda mrefu.
By PWANIFM PODCASTSUKILIMA WA MATUTA WAZALISHA CHAKULA - RUTH MASITA