Biblia Inasema Usiogope

Usifadhaike Wala Kuwa na Woga


Listen Later

Katika maisha yetu ya kila siku huwa tunapitia changamoto mbalimbali; kesi za kusingiziwa, kutafutwa na watu walighadhabika dhidi yetu, kupita katika nyakati zenye shida na mateso kwetu au watu wetu wa karibu, magonjwa yenye kutishia uhai wa wapendwa wetu, na kadha wa kadha. Haya mambo huweza kutusononesha moyo na kutufanya tufadhaike, na kufadhaika husababisha woga ndani yetu. Yesu Kristo anasema amani ametuachia, tusifadhaike mioyoni wala kuwa na woga. Kwa hiyo katika yote yanayotokea usitoke katika imani. Imani katika Kristo Yesu itakufanya ubaki na amani ya Kristo Yesu na hutafadhaika wala kuwa na woga. Kumbuka Biblia inasema usiogope.


...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Biblia Inasema UsiogopeBy Pastor Msafiri