Biblia Inasema Usiogope

Usiogope, Zinakuja Siku za Kurejeshwa


Listen Later

Katika mambo magumu unayopitia na kipindi kigumu ulichokikabili kwa muda sasa, pamoja na mateso yote yanayokusonga, usikate tamaa wala usiogope. Mungu ameahidi siku za kurejeshwa ambapo nuru itarudi usoni mwako na furaha itajaa moyoni. Ingawa ulihenya na kuwa ishara ya laana, au alama ya chukizo na kielelezo cha namna mtu anavyoweza kuporomoka, Bwana ameahidi kuinuliwa kwako mpaka iwe alama ya jinsi Bwana anavyoweza kubariki na ishara ya vile Mungu huinua. Walionyoosha kidole kwako kuonyesha aibu yako watanyoosha vidole kwako kuonyesha uzuri wako. Yote yatafanyika ili Bwana ajipatie utukufu zaidi. Ndivyo Biblia inavyosema kwako unayemtumaini Bwana Mungu, Yeye Jiwe la Israeli. Sikiliza ubarikiwe, na mshirikishe na ndugu wa karibu baraka hizi.



...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Biblia Inasema UsiogopeBy Pastor Msafiri