Sign up to save your podcasts
Or

Karibu sana kusikiliza mafundisho ya Biblia katika Wagalatia. Tunafanya mfululizo kwa waraka mzima, na hiyo ni namba 4, katika kifungu Gal 3:1–9. Hapa Paulo anaonyesha ni jambo la upumbavu kufikiri baada ya kuanza na Yesu kwa imani na Roho kwamba njia ya kuendelea au ya kukamilishwa ni kwa sheria au matendo. Anaonyesha kama Ibrahimu tunabarikiwa na kuokolewa kwa imani mwanzo hadi mwisho.
Karibu.
Mwalimu Maiki. Mchungaji Mmasa.
Soma Biblia
Gal 3:1-9
1 Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulubiwa? 2 Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? 3 Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili? 4 Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli. 5 Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? 6 Kama vile Abrahamu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Abrahamu. 8 Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiria Abrahamu Habari Njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. 9 Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Abrahamu aliyekuwa mwenye imani.
By Mwalimu Mike, Mchungaji MmasaKaribu sana kusikiliza mafundisho ya Biblia katika Wagalatia. Tunafanya mfululizo kwa waraka mzima, na hiyo ni namba 4, katika kifungu Gal 3:1–9. Hapa Paulo anaonyesha ni jambo la upumbavu kufikiri baada ya kuanza na Yesu kwa imani na Roho kwamba njia ya kuendelea au ya kukamilishwa ni kwa sheria au matendo. Anaonyesha kama Ibrahimu tunabarikiwa na kuokolewa kwa imani mwanzo hadi mwisho.