TCRA Tanzania

Wasichana katika TEHAMA, 2025: Mageuzi Jumuishi ya Kidijiti


Listen Later

Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA (International Girls in ICT Day) huadhimishwa kila Alhamisi ya nne ya mwezi Aprili kila mwaka. Hii inafuatia makubaliano ya nchi wanachama wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU),  kuhimiza wasichana kupenda kusoma masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, kwa kifupisho cha kiingereza –STEM, yaani Science, Technology, Engineering and Mathematics. Nchi wanachama wa ITU pia zilikubaliana kuhamasisha Wasichana na Wanawake kushiriki kwenye kazi za taaluma ya STEM. 

TCRA, kama mwanachama na mjumbe wa baraza la utendaji la ITU, inaendeleza jitihada na huratibu maadhimisho haya kila mwaka. Hii ni  namna mojawapo ya ya kuunga mkono jitihada za serikali na kuungana na Jumuiya ya Kimataifa katika kuwezesha watoto wa kike kupata fursa sawa na linganifu, na hasa katika TEHAMA nchini. Kauli mbiu ya mwaka 2025 ni "Mageuzi Jumuishi ya Kidijiti"


Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie [email protected]

#NiRahisiSana!

...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

TCRA TanzaniaBy Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)