Chanson Gospel en Swahili - "Quand mon Travail est Terminé".3gp / Swahili Gospel Song-"When My Work Is Over".3gp/
1 WAKORINTHO 15 - Ufufuo wa Kristo1Sasa, ndugu, napenda kuwakumbusha ile Habari Njema niliyowahubirieni, nanyi mkaipokea na kusimama imara ndani yake. 2Kwa njia yake mnaokolewa, ikiwa mnayazingatia maneno niliyowahubirieni, na kama kuamini kwenu hakukuwa bure. 3Taz Zab 53:5-12 Mimi niliwakabidhi nyinyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu; 4
Taz Zab 16:8-10 kwamba alizikwa, akafufuka siku ya tatu kufuatana na Maandiko Matakatifu; 5kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili. 6Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya 500 kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa. 7Baadaye alimtokea Yakobo kisha akawatokea mitume wote. 8Baada ya wote, akanitokea hata mimi, mimi niliyekuwa kama mtu aliyezaliwa kabla ya wakati. 9Maana mimi ni mdogo kabisa miongoni mwa mitume, na wala sistahili kuitwa mtume, kwa sababu nililidhulumu kanisa la Mungu. 10Lakini, kwa neema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa, ila ni neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami. 11Lakini hata hivyo, iwe wao ndio wahubirio au mimi nihubiriye, haidhuru, hiki ndicho tunachohubiri, na hiki ndicho mnachoamini.Ufufuo wetu