Watu hupata utambulisho wao kutokana na mambo mengi...inaweza kuwa kile wanachomiliki, maadili au imani zao. Utambulisho (Identity) sio mada mpya, ni mada ambayo ni maarufu sana kwa sababu ina athari kubwa katika maisha yetu.
Tafadhali sikiliza jinsi Bw. Mathias Masaka, ambaye ni mwanasaikolojia wa kijamii (social psychologist) na mhadhiri msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia mambo muhimu ambayo watu wanapaswa kuyafahamu kuhusu mgogoro wa utambulisho, na huku akisisitiza jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kuwa jukwaa bora la kujifunza na pia tishio kwa hisia zetu za utambulisho.