Mental Glow

08 - Mtazamo wa Afya ya Akili Jeshini ft Owden Kyambile


Listen Later

Binadamu wote huishi kwa kufanya kazi. Kazi zipo za aina mbalimbali na kila kazi ina umuhimu wa peke yake katika ustawi wa jamii. 

Kazi pekee inayotia hofu au kuleta upweke kwa binadamu, na inayoweza kuondoa uhai wa binadamu ni ya Jeshi la Mapigano. Viapo vya wanajeshi hufanywa kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu na ambaye pia ni Raisi wa nchi. Hii ina maanisha, dhamana ya wanajeshi kiutendaji ni kwa ajili ya ulinzi wa usalama wa taifa.

Jeshi la Mapigano linapoingia vitani wanajeshi wake huwa hawana uhakika kama baada ya vita watakua hai au wamekufa. Hii inapelekea majonzi makubwa sana na kibaya zaidi ni kwamba hawana muda wa kuchanganua hisia zao na hawapati msaada wa kisaikolojia kama inavyotakiwa kutokana na uhalisi wa kazi zao. 

Ungana nami katika hii episode kufahamu kiufupi historia ya vita kati ya Tanzania na Uganda na kujua zaidi kuhusiana na hali ya msaada wa kisaikolojia kwa Wanajeshi wa nchini Tanzania. Pamoja na Afisa Mstaafu, Maj. Owden Kyambile akisisitiza zaidi kuhusu kupewa kipaumbele kwa huduma za kisaikolojia kwa wanajeshi kabla na wanavyokaribia kustaafu, ili waweze kujiandaa na maisha baada ya kazi na kuepusha matatizo ya afya ya akili.

...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Mental GlowBy Jacqueline Owden