Maendelo ya Taaluma ni mchakato na sio kitu cha mara moja. Tangia utotoni, tunakuwa na matamanio ya kuwa na taaluma fulani na mara nyingi tunaishia kuwa na taaluma tofauti na tulio tamani utotoni.
Vijana wengi nchini Tanzania wanapata changamoto kwenye kuchagua taaluma inayo wafaa, na wengi wao hushawishiwa na wazazi wao kusoma masomo ambayo hawana mapenzi nayo wala kuyaweza. Hii hupelekea hofu, majuto, uzembe pindi wapo chuoni na mara nyingine changamoto ya afya ya akili.
Tafadhali ungana nami katika hii episode nikiwa na Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika taaluma ya Saikolojia, Bi. Flora Wadutya akielezea sababu ya yeye kuchagua taaluma husika, changamoto alizopitia wakati anasoma na jinsi alivyozimudu. Akisisitiza zaidi umuhimu wa mwana chuo kujitambua, kujituma, kuwa na mahusiano mazuri na watu na nidhamu katika kukuza taaluma husika.