Mental Glow

14 - Usonji | Autism ft. Hussein Mshunga


Listen Later

Mmoja kati ya watoto mia moja (1/100) duniani kote hugundulika kuwa na Usonji. Usonji huwapata wavulana mara nne zaidi kuliko wasichana. Nchini Tanzania, kumekua na elimu ndogo kuhusiana na Usonji na hii kupelekea ubaguzi kwenye baadhi ya familia zenye watoto wenye Usonji. Ungana nasi tunapo angazia ulimwengu wa watu wenye Usonji.
Katika episode hii tunaongelea maana ya usonji, jinsi ya kumgundua mtoto anaeonyesha dalili za usonji na kuelezea kiundani zaidi ya jinsi gani mzazi anaweza akamlea mtoto mwenye Usonji huku akijijali pia yeye mwenyewe.
Kupitia maswali yatakayo jibiwa na Mwanasaikolojia wa watoto, Bw. Hussein Mshunga, utapata uelewa wa ndani zaidi wa Usonji na jinsi ya kutoa msaada kwa watoto au ndugu wa karibu wenye usonji, ili waweze kutumia utofauti waliokua nao katika kuleta chachu au maendeleo katika jamii.
...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Mental GlowBy Jacqueline Owden