Tafiti zimebainisha kuwa mambo tofauti kama hali ya kiuchumi, mazingira, kujitambua, na mengineyo huathiri sana ubora wa mahusiano. Pamoja na hilo, watu wengi wamekuwa wakipata changamoto katika kutofautisha aina mbalimbali za mahusiano, na hii kupelekea mkanganyiko katika kuhusiana na watu katika mazingira tofauti tofauti.
Katika kipindi hiki, nimeungana na mwanasaikolojia tiba Mr. Nickson Kataze tukijadili kwa undani kuhusu aina tofauti za mahusiano na jinsi ya kujenga na kudumisha mahusiano bora na watu wanaotuzunguka.