Mental Glow

23 - Migogoro ya Wazazi katika Familia na Jinsi Inavyo Muathiri Mtu Mzima Ajaye ft. Barnabas Nkinga


Listen Later

Uchambuzi wa utafiti uliofanyika nchini marekani unaonyesha kuwa ongezeko la mivutano au migogoro kati ya wazazi ina uhusiano mkubwa na upungufu wa ukaribu wa kihisia kati ya mtoto na mzazi, na malezi yasiyo bora.
Watoto wanaoshuhudia mivutano au migogoro ya wazazi mara nyingi wanakabiliwa na matatizo makubwa katika mahusiano yao na pia husababisha kuvunjika kwa uhusiano kati ya mzazi na mtoto, jambo ambalo linaweza kuwa na madhara makubwa kwa mtoto, na mara nyingine hata kuathiri afya yake ya akili.
Ungana nami nikiwa na mwanasaikolojia, Bw. Barnabas Nkinga tunapoangazia na kukuza uelewa kuhusu mada hii muhimu. Haya siyo tu mazungumzo, bali ni wito wa kuchukua hatua itakayo tusaidia kulinda ustawi wa kizazi kijacho.
...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Mental GlowBy Jacqueline Owden