Changamoto za mahusiano ya kimapenzi ni moja ya sababu kubwa inayopelekea vijana wengi kutafuta msaada wa kisaikolojia. Tafiti zimeweza kuthibitisha kwamba watu wenye umri kati ya 18 - 35 ambao hawajaoa wala kuolewa, waliopitia kuvunjika kwa mahusiano yao, waliweza kupata changamoto ya afya ya akili na kupunguza kuridhika na hali yao ya maisha.
Katika kipindi hiki nimeungana na Fabian Emmanuel (Light Palmer) tukizungumza kuhusu kuvunjika kwa mahusiano (breakups) na jinsi ya kukabiliana nazo kama vijana huku tukijali afya zetu za akili na kuzingatia utimamu wa kila kitu tunachokifanya ili kufikia malengo yetu binafsi tuliojiwekea maishani.