Kila jamii ina mila na desturi zake ambazo zinakua na mchango mkubwa sana katika makuzi na malezi ya mtoto, aidha wa kiume ama wa kike. Katika kipindi hiki nimeungana na nesi mkunga, Yusra Ameir ambae ana uzoefu wa kufanya kazi na watoto pamoja na wajawazito katika sekta ya afya kisiwani Unguja.
Ungana nasi tukiongelea kiundani ni kwa namna gani baadhi ya mila na desturi za Kizanzibari zilivyo na mchango mkubwa katika kukuza unyanyasaji wa kijinsia ambao una athari kubwa kwenye afya ya akili ya mtoto wa kike na ni kwa jinsi gani serikali ya Mapinduzi inaweza ikarekebisha utoaji wa huduma katika sekta ya afya na kurekebisha miundo mbinu ya kudhibiti unyanyasaji wa kijinsia.