Katika video hii, tunachambua tafsiri mpya ya neno 'Artificial Intelligence' katika lugha ya Kiswahili ambapo sasa inajulikana kama 'akili unde'. Tunaangazia maana ya neno hili jipya pamoja na kuelezea tofauti yake na tafsiri zingine zilizokuwa zinatumika awali kama vile akili bandia, akili mnemba au akili tarakilishi. Pia, tunasisitiza umuhimu wa kufuatilia maendeleo ya istilahi za akili unde kutokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia hii.