MSINGI WA SWALI :
“Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.”
Mwa 5:1-2 SUV
SWALI:
1. Je Adamu alikuwa ni wa jinsia gani?
2. Ikiwa alikuwa ni wa kiume, Biblia imeandika "akawaita " ni wingi je mwingine alieitwa ni nani?
3. Ikiwa wote majina yao ilikuwa Adamu, Eva( Hawa) ni nani?
4. Ikiwa Mungu aliumba mtu mke na mtu mme yule mtu mke ni nani?
Katika kipindi hili ni mjadala wa utangulizi wa mjadala kamili utakaokujia kwenye kipindi kijacho.