Living Theology

HALI YA WATU KUTAZAMA TU


Listen Later

Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema, watu wote waliondoka wakasimama, kila mtu mlangoni pa hema yake, akamtazama Musa, hata alipokwisha kuingia hemani. KUTOKA 33: 8
Tunasoma kwamba Musa na mtu mmoja au wawili walizoea kwenda nje ya kambi kwenda kwenye hema kusali. Katika Kutoka 33: 8 sisi tunasoma, “Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema, watu wote waliondoka wakasimama, kila mtu mlangoni pa hema yake, akamtazama Musa, hata alipokwisha kuingia hemani. ”  Wote walichofanya ni kuangalia tu kwa hamu. Walikuwa wanajua kuwa kitu kilikuwa kinafanyika, lakini hawakujua ni nini, na hawakuielewa. Hawakutoka kambini pamoja na Musa kwenda hemani ya kukutania na Mungu na kuomba. wakishangaa kile alikuwa akifanya na nini hasa kilikuwa kinatokea.  Mahali  palipostahili pa hema kulikuwa katikati ya kambi. Lakini haikuwepo.
Unaposoma historia ya Kanisa, utapata hii kurudiwa. Mwanzoni watu wachache tu huhisi wito na kutenganisha nafsi zao. Wale wengine huaanza kusema, "Ni nini kinachotokea kwa huyo na huyo? ”
Wao wanasimama kwenye milango yao ya hema, nao wanatazama tu. Wana hisia kwamba kuna kitu kinatokea. Lakini hawafanyi chochote. Ah, ikiwa tunangoja mpaka Kanisa lote lihamie hemani, uamsho hautatokea kamwe.
...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Living TheologyBy Brendon Naicker

  • 3
  • 3
  • 3
  • 3
  • 3

3

1 ratings