InspireFikra Podcast

InspireFikra Podcast

By Mrs. Agness Gabriel SangaReligion & SpiritualitySpirituality
Download on the App Store

InspireFikra Podcast episodes

  • Karibu InspireFikra

    Episode hii inahusu utangulizi Ili upate kufahamu InspireFikra ni nini? lengo lake ni lipi na ni kwaajili ya nani?

    Nina imani baada ya kusikiliza utachukua uamuzi sahihi wa kuwa Mshirika wa kudumu wa Jukwaa hili. Utakua nami Mrs. Agnes Gabriel Sanga, Kila siku ya Jumatatu, Jumatano na Ijumaa, saa tatu kamili asubuhi. Karibu sana!

    3 min
  • Jifunze kutokana na makosa
    Ukilichukulia kosa ulilofanya leo kama funzo unaondoa uwezekano wa kurudia tena kosa hilo hilo kesho. Lakini ni ngumu kufanya hivyo kama bado unaendelea kujihukumu kwa kutenda kosa, jisamehe, kisha jifunze.
    11 min
  • Je utaweza kuishi na matokeo ya uamuzi ulioufanya leo?
    Historia ya maisha ya mwanadamu inaundwa na orodha ya maamuzi anayoyafanya leo. Uamuzi (choice) ni nguvu ambayo mwanadamu pekee ameruhusiwa na muumba wake kuwa nayo. Kama unavyowajibika kufanya uamuzi vivyo hivyo unawajibika moja kwa moja na matokeo ya uamuzi wako. Leo ninakuuliza swali ambalo naamini ukitafakari na ukalitumia ipasavyo, itakusaidia kufanya maamuzi sahihi zaidi katika maisha yako. Jaribu kabla hujafanya uamuzi wowote ule jiulize “Je nitaweza kuishi na matokeo ya uamuzi ninaoufanya?”.
    11 min
  • Je, ulipo leo ndipo ulipotaka kuwa miaka 5 iliyopita?
    Binadamu ana mipango na matarajio mengi sana, lakini wakati mwingine maisha humpeleka kwenye njia tofauti mbali na ile sehem aliyokua anatarajia kufika baada ya kipindi fulani. Je ulipo sasa ndipo ulipotarajia kuwa miaka mitano iliyopita? Kama sivyo, unafanyaje? Agness anaongele hili kwenye episode ya kwanza ya Inspire Fikra. Karibu
    6 min
  • Thubutu kuota/Dare to Dream
    Karibu. Huu ni muhtasari wa mengi mazuri na yakuhamasisha ninayotarajia kukushirikisha kupitia Podcast hii. Tunaanza na NDOTO, maana kila jambo zuri na la kushangaza unaloliona hapa duniani limesababishwa na mtu mmoja aliethubutu kuota. Ilhali pumzi bado unayo basi haujachelewa, thubutu kuota.
    1 min

About InspireFikra Podcast

From the publisher's feed

Je, wewe ni Mfanyabiashara, Mfanyakazi wa Taasisi ya Umma/binafsi au ni  Mwanafunzi? Je, umekuwa ukihisi kuna kitu kinakosekana katika maisha yako na katika kazi unayofanya? Huenda huo ukawa wito…