Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. WARUMI 10: 2
Wayahudi walikuwa wanatarajia kuja kwa Masihi, lakini hawakumtambua Yeye alipokuja. Walikataa njia moja ambayo kwayo wanadamu wanaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu.
Paulo alisema "Ninawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. ” Wapuuza kuzingatia mwanga na maarifa ambayo Injili ingeweza kuwapa kitu walicho tamani. Sio kwamba walikosa bidii, lakini kwamba waliiamini walikuwa na haki ya lazima kwa sababu ya bidii yao. “Wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. ” Kwa kweli, walikataa maarifa ambayo Injili ilikuwa ikiwapatia kwa kuzingatia bidii yao". Hapa kuna mgongano wa bidii na maarifa. Mgogoro kati ya uaminifu na ukweli.
Sifa hizi -bidii na uaminifu- zinainuliwa katika siku zetu haswa kama walivyokuwa Wayahudi wa zamani. Maarifa yanapunguzwa thamani, na kudharauliwa. Uwazi, na ufafanuzi halisi wa Maandiko umepuuzwa. Mafundisho huchukuliwa kama adui wa ukweli, na hata matendo mema hayapewi umaarufu yaliokuwa nayo miaka michache iliyopita. Hii ikiwa sababu ya juhudi iliyopotoka.