Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule;akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yafa ukamwite Simoni aitwaye Petro, atakayekuambia maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote. Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.
MATENDO 11: 12-15
Angalia kwamba Petro anasema Roho Mtakatifu aliwashukia Kornelio na nyumba yake "kama alivyotushukia mwanzoni." maana yake, "Alivyowapata ndivyo ilivyotupata Siku ya Pentekoste. ” Kwa maneno mengine, ubatizo wa Roho Mtakatifu ulitendeka Siku ya Pentekoste, lakini pia ulifanyika baadaye kwa Kornelio na nyumba yake. Hiyo ndiyo hoja ya Petero: “Ndipo nikakumbuka neno la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana kweli anabatiza kwa maji; lakini mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu. Kwa kuwa basi, kama Mungu “alivyofanya kwetu sisi, tuliomwamini Bwana Yesu Kristo; mimi nilikuwa ni nani hata kumhimili Mungu? ”
Lazima tukome kusema kwamba kile kilichotokea Siku ya Pentekoste kilitokea mara moja tu. Jambo hilo lilitokea baadaye kwa njia ile ile wakati Petro alikuwa akiwahubiria Kornelio na nyumba yake. Roho Mtakatifu aliwashukia kama alivyowashukia wale watu katika chumba cha juu huko Yerusalemu.