Je, umewahi kukosa kuomba kazi kwa sababu tangazo lilihitaji uzoefu wa miaka 3 au zaidi? Kama ndiyo, basi episode hii ni kwa ajili yako.
Wahitimu wengi hujikuta kwenye mzunguko wa kutaka kazi lakini wanakosa uzoefu, huku waajiri wakitaka uzoefu kabla ya kutoa nafasi ya kazi. Habari njema ni kwamba uzoefu haupatikani kupitia ajira rasmi pekee. Unaweza kuujenga mwenyewe na kuutumia kujiongezea thamani kwenye soko la ajira.
Katika episode hii ya Me & The Graduates Podcast, tunazungumzia njia 8 za vitendo ambazo graduate anaweza kutumia kujijengea uzoefu, kuimarisha CV yake, kujenga mtandao wa kitaaluma, na kuongeza nafasi za kupata kazi au fursa nyingine za maendeleo.