Hakuna mtu amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, isipokuwa Mwana, na yeyote Mwana apenda kumfunulia. (MATHAYO 11:27)
Kando na Wokovu kuniletea maarifa ya msamaha, kusamehewa, na kupatanishwa na Mungu; Zaidi ya yote, inatupa ujuzi na maarifa ya Mungu.
Fikiria haya! Umewahi kuona urefu na kimo cha Injili ya Yesu Kristo? Kwa Injili twapewa ujuzi wa Mungu wa mbingu na ardhi, Muumba, mtunzaji wa kila kitu kilichoko. Nawezaje kumjua Mungu asiye na mwisho, aliye kamili, na wa milele — na nimjue Yeye kama Baba yangu — hii ndio ufunuo katika Mathayo 11:25.
Ufunuo kwamba sisi ni Wana, naye ni Baba. Ndivyo Bwana wetu alikuwa anasema: kwamba sisi, ingawa tumetenda dhambi, katika wokovu, tunakuwa ndani yake wana wa Mungu, warithi wa mbinguni na ya furaha milele na milele.
Niulize hivi - ni nani isipokuwa Mungu angeweza kuifikiria jambo hili? Kwa njia ya kushangaza sana, katika uchi wetu kabisa na kwa kukosa msaada; Yeye huvuta tu nyuma pazia na hutufunulia jinzi alivyo kikamilifu katika Yesu Kristo. Yeye ni wokovu kamili, “kwa Mungu alifanywa kwetu sisi hekima, na haki, na utakatifu, na ukombozi ” (1 Wakorintho 1:30) - . Sisi sote tunapaswa kumtazama Bwana Yesu Kristo na kuamini rekodi hii kumhusu Yeye. Tujisalimishe kwake na tukubali zawadi hiyo, nasi tutamjua Bwana wa mbingu na dunia kama Baba wetu.