Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.
1 TIMOTHEo 2: 8
Sharti la tatu kuhusu sala ni "bila shaka ” Kwa maneno mengine, "bila majadiliano. " Rejeleo sio kujadiliana na wengine, lakini kujadili mwenyewe. Inaashiria hali ya kuyumba yumba na kutokuwa na uhakika. au hata uasi wa kiakili.
Shaka inaweza kujieleza kwa njia nyingi tofauti. Tunawezekana kuwa na shaka kwa uhai wa Mungu. Shaka, hutumia maneno kama; iwapo "yeye [Mungu] yupo. ” Halafu kuna mashaka pia juu ya nguvu au uwezekano wa maombi. Je..! kitu chochote kinaweza kutokea au hata hufanyika katika kuomba kwetu?
Matokeo ya mashaka ni kukata tamaa. Katika hali hii tunajikuta katika wakati mgumu; Sisi "tunapiga kelele gizani," Tusipo zingatia hali hii ya tatu, sala haina maana. Sisi lazima tumwendee Mungu tukiamini “kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. ”(Waebrania 11: 6). Wanadamu ambao maombi yao yamejibiwa daima ni wale waliomjua Mungu. Ambao wamemwamini kabisa. Walio tayari kusema kila wakati na katika hali zote, “Mapenzi yako yatimizwe”, wakiwa na uhakika na upendo wa Mungu. Wasio na shaka, bila ubishi, bila kukata tamaa, lakini badala yake kupumzika kwa utulivu ndani ya Mungu mwenye Uvumilivu na mapenzi kamili.