Learn Swahili with SwahiliPod101!
Don't forget to stop by SwahiliPod101.com for more great Swahili Language Learning Resources!
-------Lesson Dialog-------
----Formal ----
UKOO FLANI MAU MAU
Kalamashaka ni kikundi cha hiphop ambacho kinapatikana katika makaazi duni ya Dandora, Nairobi, nchini Kenya.
Kikundi hiki kiliundwa na Johnny, Kama, na Oteraw mnamo wa miaka ya kati ya tisaini.
Kikundi hiki kimewasaidia vijana wa Dandora kwa kuaanzisha kazi katika muziki wa kufoka.
Pia waliunda kikundi cha Ukoo Flani Mau Mau , ambacho ni mkusanyiko wa wasanii 24 kutoka Mombasa, Nairobi na watu kadhaa kutoka Tanzania.
Kuongezea, wameheshimika kwa sababu ya kuwainulia pazia wasanii kutoka nchi za ngambo ambao hukuja kututumbuiza humu nchini kama Lost Boyz na Coolio.
Pia wameimba pamoja na kikundi cha Dead Prez na wanamuziki wengine wa kimataifa.
Ukoo Flani ilitengenezea njia nyimbo za Kiswahili za kufoka na hiphop na kuzifanya kuwa na muundo mpya nchini.
Kikundi hiki kinaumaarufu kwa wafuasi wake wa kufoka kwa ajili ya ujumbe wao unaozingatia siasa na jamii.
Katika mwaka wa 2001, walitoa rekodi yao ya kwanza na wimbo 'Ni Wakati', ambao ulivuma sana nakutengenezea njia nyimbo, 'Fanya Mambo' and 'Tafsiri Hii' ambazo zilikuwa maarufu zaidi na kuwafanya wajulikane kiasi.
Wamefanya maonyesho katika nchi nyingi kama Afrika Kusini, Usudi, Norwei, Uholanzi na Nigeria mwiongoni mwa nchini nyingine.
Wana hali ya kipekee, ladha na nguvu inayotokana na makao yao ya kipekee inayowaunganisha pamoja na ujumbe chini ya kipaji cha hiphop.
Hata hivyo, umaarufu wao ulianza kudidimia kutokana na kuibuka kwa kikundi cha genge na kapuka ambayo ingesakatwa kwa urahisi na vijana ambao asilimia yao kubwa huipenda badala ya miziki ya falsafa.
Stesheni za redio pia zimepunguza kucheza miziki ambayo yana maadili ya kijamii kama ilivyo kawaida ya Ukoo Flani.
Jambo hili lilichangia sana kupunguka kwa umaaarufu wa Ukoo Flani.
Hata hivyo, wamebaki wima na kukataa kubadilika na wakati ili kufanya miziki ya kibiashara.
----Formal English----
Ukoo Flani Mau Mau
Kalamashaka is a hip-hop group that is based in the ghetto estate of Dandora in Nairobi, Kenya. The group was formed by Johnny, Kama, and Oteraw in the mid-90s. This group has helped other youths of Dandora in starting up their careers in rap music. They also formed the group Ukoo Flani Mau Mau, a collection of 24 rappers from Mombasa, Nairobi, and some Tanzanians. The group has had the honor of curtain raising for international rap stars that come to perform in the country, like the Lost Boyz and Coolio, and they have also done collaborations with Dead Prez and many other international artists. Ukoo Flani paved the way for Swahili rap and hip hop and made it become the new trend in Kenya.
Ukoo Flani Mau Mau is popular to their fans with hardcore rap music and also for their politically and socially conscious lyrics. They released "Ni Wakati," their first album, in 2001, which became a hit and saw them rise to fame due to their hit songs "Fanya Mambo" and "Tafsiri Hii." They have performed in many countries, like South Africa, Sweden, Norway, the Netherlands, and Nigeria, among many others. They have the uniqueness, flavor, and power that come from many unique backgrounds and unite them with a message under the hip-hop banner. Their popularity, however, started to fade away with the rise of Genge and Kapuka, which were more danceable, which a huge percentage of youths enjoy and prefer to listen to rather than listening to philosophical music. Radio stations have also become reluctant to play music that is socially conscious, which is typical of Ukoo Flani, which led to their fall from being famous. The group has, however, remained active and has refused to change with the current times and refused [...]