. . . hakuna mtu amjuaye Mwana, ila Baba. MATHAYO 11:27
Bwana wetu anadai kwamba yuko katika uhusiano wa kipekee na Mungu katika kumfahamu . "Hakuna mtu," Anasema, "amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana. ” Kwa maneno mengine, anasema “Mnaniona Mimi, lakini hamnijui Mimi. Anayenijua Mimi ni Mungu pekee, na mimi ndiye peke yangu, ambaye ninamjua Mungu. Mnaomba, mnazungumza na Mungu, lakini hamumjui Mungu kama mimi.
” Hakuna mtu "aliyemwona Mungu wakati wowote," wala kuona umbo lake. Lakini Kristo alisema kwamba amemwona, na alidai, kama Wayahudi walivyotambua, usawa na Mungu Baba. Alijiweka hapa kwa hapa(pamoja) na Mungu. “Je! Mnajua kwamba ulimwengu wote huu, mbingu na ardhi na kuzimu na vitu vyote — zimekabidhiwa kwangu Mimi na Mungu Baba? ” Hayo ndiyo madai yake: uwana wa kipekee, uhusiano wa kipekee na Mungu, na uhusiano wa kipekee na ulimwengu huu. Kamwe ulimwengu haujawahi kuona au kusikia mtu yeyote ambaye amedai hivi. Yeye ni nani, huyu anayedai kwamba Yeye kweli ni Mwana wa Mungu?
Huyu ndiye mwana wa pekee wa Mungu mwokozi wetu ambaye alifunuliwa kimiujiza. (1 Timotheo 1:16)