Ibada ya Tarehe 21/1/2024
Sermon Summary
Mch: Ephraim Mbila.
1Samweli 25
Habari ya Nabali.
Somo: Shukurani ya Punda ni Mateke.
Nabali alikua ana mifugo yapatayo 4,000 na wachungaji. Daudi alipokua eneo alilokua akifanya machungi aliweza pia kufanyika ulinzi wa mifugo yake pamoja na wachungaji wa mifugo yake.
Maana ya jina Nabali - mtu Mpumbavu
“a Fool”. Ijapokua alikua na mali nyingi lakini alikua mtu muovu,aliyekosa adabu. Ijapokua ni mtu mpumbavu na muovu Alipata mke mzuri Abigail -maana ya jina lake “furaha ya baba yake.”
Abigail aliutambua udhaifu wa mume wake na kwa hekima aliufunika.
Katika habari iliyo katika kitabu hiki, Inafika kipindi cha Mavuno kwa Nabali na Daudi awatuma vijana wake kwa Nabali kwamba aweze kumpa chochote kwa ajili ya jeshi lake na yeye. Majibu ya Nabali yatoka kwa kiburi na yenye jeuri na anasisitiza kua hamtambui Daudi, wala kazi ile ya ulinzi Daudi na Jeshi lake waliofanya kwa mifugo na wachungaji wake.
Tutafakari Mungu anapokuja kwetu na yeye ndiye aliyetupa yote tulionyayo si kwa kustahili bali kwa neema yake.
Je tunajibu nini?
Mfano:(Mafuriko haya yaliyoleta maafa makubwa na upotevu wa maisha je ni nini cha ziada tulichofanya kustahili kua salama?)
Ni wachache huingia kwenye maombi kuomba walivyonavyo iwe ni watoto,ni kazi ni elimu. Je ni kweli kwamba vyote tuliomba kwa Mungu ndio maana amekupa au Je ni kweli kua vingi ambavyo tunavyo tumejikuta tumevipata.
Ni kweli pia kua kuna ambavyo tumeomba na hatujapata kwa kua tunaomba vibaya kwa ajili ya tamaa zetu wenyewe. Ila ni mengi Mungu hututendea na bado tumekua wenye kiburi kutambua ya kua vyote tulivyo navyo ni kwa utukufu wake.
Mfano wa mchungaji: “Nimepaki V8 nje ya kanisa ili kila atakaeulizwa ajibiwe ni la Mch: Mwakajangwa , wanikome na waniheshimu”
Bila Mkono wa Mungu aliye Hai haiwezekani kufanikiwa. Si kwa ujuzi wala uwezo tulionao tusiwe wapumbavu kama Naabali “a fool”
Je Tunajibu nini tunapotakiwa kuwatunza watumishi wa Bwana? Hua tunajibu nini?
Tumeongea maneno ya jeuri na maneno magumu kwa watu. Kama nabali tumejibu majibu magumu na yasiyofaa mbele za Mungu.
Jibu la Daudi;
Anachukua Silaha na jeshi zima kwenda kumaliza familia ya nabali wala hakuna ataesalia. Ni kwa kiburi chake ameleta uangamivu kwenye familia yake. Japo Abigail kwa hekima aliweza kuzuia hilo Nabali alikufa kwa ugonjwa wa moyo.
Siri kubwa ni mkono wa Mungu kwenye maisha yetu unapotoweka basi shetani huchukua nafasi.
Mungu ni Mungu mwenye hasira ingawa biblia inasema si mwepesi wa Hasira bali ni mwingi wa rehema. Tusiwe kama Nabali mpumbavu na kupelekea Mungu kuchukua kiti cha hukumu kwenye maisha yetu.
Neno la Mungu ni amri, maneno ya Mungu ni maagizo ni katika utii ndipo tutaweza kutenda sawa sawa.
Tafakari
Je yawezekanaje mtu kulalamika wazi juu ya maombi kanisani?
Je yawezekanaje mtu kupinga waziwazi ajenga za Mungu kanisani hasa juu ya utoaji?
-“Kwanini tutoe ujenzi?”
“Kwanini tutunze madhabahu?”
“Kwanini tuchangie wagonjwa?”
“Kwanini huu msiba tuchange?”
Maombi ni muhimiri wa kanisa , ni vyema kua na akili na kutambua hawa watu wenye maswali yapingayo agenda za Kimungu ni chanzo cha uharibifu kanisa, Na kama “upumbavu” wa Nabali kupeleka anguko letu.
Luka 7:1-10
Habari ya akida aliyepata uponyaji kwasababu ya mema aliyofanya kwa taifa la israel na ujenzi wa Sinagogi.
Funzo: katika kutoa kwake aliweza kupata kibali cha kusikilizwa na habari yake kufikishwa kwa Yesu na kupata uponyaji.
Kuelekea sikukuu ya uwakili tukaseme Mungu asante kwa yote aliyotupa na tukatoe sawasawa na uaminifu wetu kwa Mungu. Tuachane na uoga wa maisha haya vinywa vyetu visiwe vyepesi kutamka madhaifu “Januari ni mwezi dume” tukiri maneno ya Mungu wakati wote bila kuangalia mazingira.
Mwanakondoo Ameshinda.