Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. 2 Wakorintho 12:9-10
Kwa wale walio katika mwisho mfano wa giza ndio, uwepo wa Mungu umekuwa halisi zaidi na utambuzi wa nguvu ya kudumisha kwake katika yote imekuwa dhahiri.
ushuhuda miongoni mwa Wakristo huko Ujerumani ambao walipitia shida ngumu kwa sababu ya imani yao ni kwamba; ilikuwa bora kwao kushriki mambo haya yote, na kwamba walimshukuru Mungu kwa ajili ya shida hizo. Kupitia mambo haya waliwezeshua kutambua umaskini wa maisha yao ya Kikristo na uzoefu wao;kupitia vitu hivi pia walikuwa wamefumbuliwa macho yao kwa "maajabu ya neema yake." Hiyo ni njia yao ya kisasa ya kuelezea kile katika Zaburi twasoma hivi: "Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa, Nipate kujifunza amri zako.”(Zaburi 119: 71).
Paulo katika ugumu wake alijibiwa na Mungu kwamba, "Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu". Jibu la Paulo likawa "Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.”(2 Wakorintho 12: 9-10).
Ikiwa tutampenda Mungu na tujitiishe kwake, kwa hakika nia yetu itakuwa vile vile; kwa maana ningekumbusha tena kwamba “vitu vyote hufanya kazi pamoja kwa uzuri kwa wale wampendao Mungu, kwa wale walioitwa kulingana na kusudi lake.”