MAELEZO PODCASTS

MAELEZO PODCASTS

By Tanzania Information Services Department (Idara ya Habari-MAELEZO)NewsEducationGovernment
Download on the App Store

MAELEZO PODCASTS episodes

  • Utafiti Kuhusu Kiwango cha Pombe na Athari Katika Moyo

    Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Richard Kisenge kuhusu ushiriki wa JKCI katika michuano ya AFCON ambapo taasisi hiyo inatarajia kutoa huduma kwa teknolojia ya kisasa na mpya barani Afrika, pia kutoa taarifa ya utendaji na mafanikio ya taasisi katika kuwafikia wananchi.

    Support the show

    Msemaji Mkuu wa Serikali

    1 hr
  • Simulizi ya Mpiga Picha Aliyefanya Kazi na Marais Wote Tanzania

    Mazungumzo na Mzee Hokororo, Mtumishi Mstaafu wa Idara ya Habari-MAELEZO anayesimulia historia ya Idara, safari ya sekta ya habari nchini mpaka kuanzishwa kwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na safari yake ya umahiri katika upigaji picha iliyomuwezesha kufanya kazi na marais wa awamu tofauti kuanzia Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hadi awamu ya sita.

    Support the show

    Msemaji Mkuu wa Serikali

    54 min
  • Huduma ya Mama Kujifungua Bila Maumivu Yaanza Kutolewa Tanzania

    Dkt. Lugano Wilson, Daktari Bingwa wa usingizi na ganzi tiba kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodona anatupitisha zaidi kwenye hduma hii kuanzia historia yake, sababu za kuanzishwa kwa huduma hii ya uzazi, faida yake, malengo ya huduma hii kwa miezi sita ya kwanza na usalama wa huduma hii kitaalamu ikifahamika epidural.

    Support the show

    Msemaji Mkuu wa Serikali

    28 min
  • Si kila mtu au kila mahali unaweza kurusha droni, kwa nini?

    Mazungumzo na mkaguzi wa droni (Drone Inspector), Bw. Ibrahim Abdallah kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ambaye ameweka wazi kuhusu taratibu za usajili wa droni na utaratibu wa kufuata ili mtu aweze kupata leseni ya kurusha droni.

    Unaweza kutazama Episode hii pia kupitia chaneli ya Youtube "Maelezo TV".

    Support the show

    Msemaji Mkuu wa Serikali

    45 min
  • Je, Tanzania atahodhi mchezo gani AFCON, Ufunguzi au fainali?

    Mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa kama vile maandalizi ya AFCON 2027, mipango ya serikali kuhusu mvua za El Nino, maadili na miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

    Support the show

    Msemaji Mkuu wa Serikali

    43 min
  • Tahadhari ya Mvua za El Niño Kuanzia Oktoba, 2026

    Kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) juu ya uwepo wa mvua kubwa za El Nino, kupitia Maelezo Podcast ili kupata ufafanuzi tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a ambaye anaeleza kuhusu mvua hizi zinavyotokea na tahadhari za kuchukua.

    Support the show

    Msemaji Mkuu wa Serikali

    57 min
  • Aina Tatu za Saratani Zinazoathiri Maisha ya Wengi Nchini.

    Katika kujenga uelewa kuhusu ugonjwa wa saratani, kupitia Maelezo Podcast tumemualika Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dkt. Chrispin Kahesa, tumezungumza kuhusu saratani na namna inavyoathiri makundi mbalimbali katika jamii, jitihada za kuzuia na tiba ya saratani.

    Support the show

    Msemaji Mkuu wa Serikali

    52 min
  • Changamoto ya Afya ya Akili, ni Akina Nani Waathirika Zaidi?

    Kupitia Maelezo Podcast tunajadili kuhusu afya ya akili kwa kumualika Daktari Veronica Lyimo, Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili kutoka Taasisi ya Afya ya Akili Tanzania, ambaye anatupitisha kwenye visababishi vya changamoto ya afya ya akili, dalili, utofauti wa ugonjwa wa akili na changamoto ya afya ya akili na namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

    Support the show

    Msemaji Mkuu wa Serikali

    1 hr 5 min
  • Kwanini ni marufuku kutunza kwa kutupa fedha chini?

    Mazungumzo na Bw. Atufigwege Mwakabalile, Afisa Mwandamizi wa Benki kutoka Benki Kuu Tanzania (BOT) kuhusu sheria ya fedha nchini na marufuku iliyotilewa ya kutotunza fedha kwa kutupa chini.

    Support the show

    Msemaji Mkuu wa Serikali

    58 min

About MAELEZO PODCASTS

From the publisher's feed

Sikiliza MAELEZO PODCASTS (Podcasts za Kiswahili kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Tanzania) kupata taarifa na matukio mbalimbali nchini Tanzania. Idara ya Habari (MAELEZO) ipo chini ya Wizara ya…