Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

03 MEI 2024

05.03.2024 - By United NationsPlay

Download our free app to listen on your phone

Download on the App StoreGet it on Google Play

Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira. Pia tunakupeleka nchini Somalia na Jamhuri ya Kidemcrasia ya Congo, kulikoni? Hii leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na shirikisho la waandishi wa habari duniani, IFJ wametoa ripoti yao ikionesha kuwa ni katika kipindi cha miaka 15 iliyopita waandishi wa habari 44 waliuawa wakiwa wanachunguza masuala ya mazingira. Kampeni ya siku hii ni kwamba kila habari kuhusu mazingira lazima isimuliwe hivyo waandishi wa habari walindwe.Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi.Katika makala tukisalia na siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, namkaribisha Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira.Na mashinani tutaeleke nchini Jamhuri ya Kidemcrasia ya Congo kufuatili jinsi ambavyo mashirika wanavyohaha kusaidia waathirika wa miozo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu

More episodes from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu