Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

07 MEI 2024

05.07.2024 - By United NationsPlay

Download our free app to listen on your phone

Download on the App StoreGet it on Google Play

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako Umoja wa mataifa uko mstari wa mbele kuwapa msaada wakenya wanaotatizika kutokana na mafuriko. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kuhusu Gaza, Uhamiaji na misitu. Mashinani inatupeleka nchi Haiti, kulikoni? Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerejea kusisitiza wito wake wa kusitishwa mapigano, kuachiliwa kwa mateka wote na kuepusha zahma kubwa ya kibinadamu kwa watu wa Gaza. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani amesema “Tuko katika wakati maamuzi kwa ajili ya watu wa Palestina na Israeli na kwa hatima ya Ukanda mzima.Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM leo limezindua Ripoti ya Dunia ya Uhamiaji 2024, ambayo inaonyesha mabadiliko makubwa katika mifumo ya uhamiaji duniani, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao na pia ongezeko la fedha zinazotumwa kimataifa. Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope amezindua rasmi ripoti hiyo nchini Bangladesh, nchi ambayo iko mstari wa mbele katika changamoto za uhamiaji na kusema "Ripoti ya Uhamiaji Duniani ya 2024 inasaidia kuondoa utata wa uhamaji wa binadamu kupitia takwimu na uchambuzi unaozingatia ushahidi." Kati ya mwaka 2,000 na 2022 ongezeko la utumaji fedha nyumbani kimataifa kwa mujibu wa Ripoti lilikuwa ni zaidi ya asilimia  650 na kufikia dola bilioni 831 bilioni.Na jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu misitu kikao cha 19 kinaendelea hapa kwenye makao makuu wa Umoja wa Mayita New York Marekani kikimulika mada mbalimbali ikiwemo jukumu la sheria katika afya ya misitu. Akizungumzia hilo Patricia Kameri-Mbote mkurugenzi wa idara ya sheria katika shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP amesema “Misitiu ni muhimu sana katika kushughulikia majanga matatu makubwa yanayoikabili Dunia ambayo ni uchafuzi wa hewa, opotevu wa bayoanuwai na mabadiliko ya tabianchi.” Na kwamba afya ya misitu ni nguzo ya kuhakikisha afya ya sayari dunia na kwa mantiki hivyo sheria za kulindwa kwa misitu zina wajibu muhimu sana na sio chaguo bali ni lazima.Na mashinani huku kukiwa na ghasia zinazoendelea nchini Haiti, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limepanua kwa haraka msaada wake wa chakula, na kufikia zaidi ya watu nusu milioni tangu kuanza kwa mzozo, ikiwa ni pamoja na watoto wa shule, Evenie Joseph, mama mjasiriamali anasema mpango wa mlo shuleni umeleta manufaa kwa watoto wanaokimbia ghasia hizo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

More episodes from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu