Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 MEI 2024

05.09.2024 - By United NationsPlay

Download our free app to listen on your phone

Download on the App StoreGet it on Google Play

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika kazi za Zahra Salehe na timu yake ya ICCAO nchini Tanzania katika kusongesha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kuhusu Gaza na asasi za kiraia Nairobi Kenya, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki. Leo mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia umeng’oa nanga mjini Nairobi Kenya ukiwaleta pamoja washiriki takriban 1500 kutoka kila kona ya dunia wakifanya majadiliano ya awali na kutoa takwimu kuelekea mkutano wa wakati ujao utakaofanyika New York Marekani mwezi Sepemba mwaka huu. Umoja wa Mataifa Kenya ndio mwenyeji wa mkutano huo ambapo Mratibu Mkazi wa Umoja huo nchini humo Dkt. Stephen Jackson amesema taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa mstari wa mbele kwenye kusongesha ushirikiano wa kimataifa tangu uhuru wake.Huko Gaza takriban watu 80,000 wamekimbia Rafah tangu Jumatatu wiki hii wakati mashambulizi ya Israel yakishika kasi usiku kucha kuamkia leo ndani na katika viunga vya vya mji huo a Kusini mwa Gaza kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Na kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adili na Idili.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

More episodes from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu