Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

10 MEI 2024

05.10.2024 - By United NationsPlay

Download our free app to listen on your phone

Download on the App StoreGet it on Google Play

Hii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) unaofunga pazia leo, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa hotuba yake kwa waandishi wa habari, na tutasikia ujumbe wa washiriki wengine. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa. Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitamatika leo, miongoni mwa waliohudhuria ni Ally Mwamzola kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA Tanzania). Amezungumza na Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa, UNIS nchini Kenya na anaanza kwa kumweleza waliyowasilisha.Na katika mashinani tunasalia mjini Nairobi katika mkutano wa asasi za kiraia kusikia ujumbe kuhusu janga la mafuriko yanayoendelea nchini Kenya.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

More episodes from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu