Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 MEI 2024

05.15.2024 - By United NationsPlay

Download our free app to listen on your phone

Download on the App StoreGet it on Google Play

Hii leo jaridani tunaangazia machafuko Gaza, na ziara za Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing. Makala tunakupeleka mjini Manama huko Bahrain na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kuonya kuhusu hali mbayá ya Rafah Gaza ambako mashambulizi ya Israel yanaendelea kukatili Maisha ya watu na kulazimisha maelfu kufungasha vitago tena kwenda kusaka usalama. Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing ameendelea na ziara yake ya kuwaaga viongozi wa eneo hilo na sasa ametembelea Somaliland.Makala tunakwenda Manama mji mkuu wa Bahrain huko Asia ya Magharibi kunakofanyika mkutano wa tano wa Jukwaa la Uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 ambapo Assumpta Massoi amezungumza na mjasiriamali kutoka Kenya, Edith Lewela, Mwenyekiti wa kundi la wanawake wajasiriamali wa Taita-Taveta. Yeye ni mnufaika wa  mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na UNIDO mwaka 2009, sasa anafundisha wenzake.Mashinani tutaelekea katika mitaa ya mabanda ya Nairobi nchini Kenya      kusikia ni kwa jinsi gani Umoja wa Mataifa unatumia michakato ya kiteknolojia ya kompyuta  kutoa msaada wa chakula kwa wakati.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

More episodes from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu