Anna anarejea mwaka 2006 na anagundua, mchungaji Kavalier ametekwa nyara. Kwa kuwa hana uwezo wa kujua aliko mchungaji, Anna anaelekea tisa Novemba, 1989, usiku ambao Ukuta wa Berlin ulianguka.
Mwaka 2006, Paul anamwambia Anna kuwa mchungaji ametoweka. Mwanamke mwenye mavazi mekundu amemteka nyara. Paul bila shaka anajua mambo mengi kumuhusu Mchungaji Kavalier na mtambo wa wakati, lakini hana muda wa kuzungumzia hayo. Anna anakubali kuelekea usiku wa tarehe 9 Novemba mwaka 1989 wakati wakazi wa Berlin walipokuwa wakisherehekea kuanguka kwa Ukuta. Anataka kuliopoa kasha kutoka katikati ya kundi la watu.