Bila kufanya maamuzi ya kumwamini Mungu katika eneo la fedha na uchumi wako kwa kutegemea neema yake, utaendelea kutaabika kila siku pasipo kuona mwanga wa kazi kamilifu ya Msalaba. Katika mfululizo wa somo hili Mwalimu Huruma Gadi anafundisha namna ya kuishinda hofu na kuchukua hatua ya imani kwa kuanza kumtegemea Mungu katika fedha zako na uchumi wako.