
Sign up to save your podcasts
Or


BURN THE BRIDGE.
Kuna wakati kwenye maisha unatakiwa kuacha kabisa njia ya kurudi kwenye mtu uliyekuwa.
Tabia za zamani. Marafiki wanaokurudisha nyuma. Mazoea yanayokumaliza. Comfort zone. Maisha yasiyo na direction.
Ukishavuka, usiache mlango wa kurudi wazi.
Kwa sababu kila unapojaribu kujenga maisha mapya, maisha yako ya zamani yatajaribu kukuita urudi.
Usipokee simu.
Hii siyo kuhusu kuwachukia watu au kujiona bora kuliko wengine.
Ni kuhusu kujilinda dhidi ya kile unachojua tayari kinakuzuia kuwa mtu unayetaka kuwa.
Burn the bridge. No way back. Only forward.
#MwanaHisabati #ArthurGeil #Mindset #Mafanikio #MbeleYaMuda
Maisha yana pande mbili kuna nyakati unapanda na kuna nyakati unaanguka.
Leo unaweza kuwa juu, kesho ukajikuta unaanza upya. Lakini kuanguka hakumaanishi umefeli, wakati mwingine ni sehemu ya safari ya kujenga maisha bora.
Kwenye episode hii tunazungumza kuhusu kwa nini maisha hayana sare, kwa nini mafanikio yanahitaji kulindwa, jinsi ya kujinasua unapojikuta kwenye “negative side” ya maisha, na kwa nini experience unayoipata baada ya kuanguka inaweza kuwa silaha yako kubwa.
Usiogope kuanza tena. Muhimu ni usikubali chini kuwa makazi yako.
#Mwanahisabati #Maisha #Mafanikio #Mindset #Psychology
NINI KITATOKEA KABLA YA KUYAFIKIA MAFANIKIO YAKO? 🎙️
Kabla hujafika kwenye maisha unayoyaota, kuna kipindi ambacho utajiuliza kama kweli uko kwenye njia sahihi.
Utakutana na rejection. Utapoteza pesa. Utapoteza watu. Utaona wengine wanakupita. Utafanya kazi bila kuona matokeo. Na kuna muda utaanza kujiuliza kama kweli unaweza.
Tatizo ni kwamba, wengi huchukulia temporary defeat kama permanent failure.
Wanashindwa mara chache, wanaona wamefeli. Wanajaribu biashara, haifanyi vizuri, wanaacha. Wanaanza kujenga kitu, hawapati attention, wanakata tamaa. Wanapitia kipindi kigumu, wanaamini maisha yamewaambia “hii sio njia yako.”
Lakini vipi kama hicho kipindi hakijaja kukuambia uache?
Vipi kama kimekuja kukufundisha, kukujenga na kukuandaa kwa kile unachokisaka?
Katika episode hii tunazungumzia mambo ambayo yanaweza kutokea kabla hujafikia mafanikio yako, kwa nini kushindwa hakumaanishi safari imeisha, na kwa nini unatakiwa kujifunza kuanza tena unapopigwa na maisha.
🎧 NINI KITATOKEA KABLA YA KUYAFIKIA MAFANIKIO YAKO!
Sikiliza episode hii mpaka mwisho.
Na ukumbuke:
Temporary defeat si mwisho wa safari.
— MWANAHISABATI Arthur Geil
Je, kweli maisha yanaweza kubadilika ndani ya wiki mbili?
Katika episode hii ya kwanza, tunazungumzia kwa nini watu wengi hushindwa kubadilika si kwa sababu hawana uwezo, bali kwa sababu hawadumu kwenye hatua mpya kwa muda wa kutosha. Utajifunza jinsi tabia ndogo za kila siku zinavyoanza kuijenga akili yako, kuunda utambulisho mpya, na kuweka msingi wa mabadiliko makubwa ya muda mrefu.
Hii si ahadi ya miujiza. Ni mazungumzo kuhusu nguvu ya consistency, nidhamu, na kuamua kuanza leo badala ya kusubiri siku na wakati sahihi.
Ukimaliza kusikiliza episode hii, utakuwa na mtazamo mpya kuhusu:
Kama unapenda maudhui ya mindset, nidhamu, maendeleo binafsi na kujenga maisha bora, hakikisha umefollow podcast hii ili usikose episode zinazofuata.
Safari ya kujibadilisha inaanza leo.
From the publisher's feed
MWANAHISABATI ni personal development brand inayozungumzia maisha kama yalivyo, mindset, psychology, discipline, habits, money, philosophy, human behavior na mambo mengine…
Ninapenda kuchimba ndani ya ideas, research, vitabu na life lessons mbalimbali, kisha kuzileta kwenye lugha rahisi na maisha halisi. Sio motivational talk tu bali ni kujaribu kuelewa kwa nini tunafanya tunachofanya, kwa nini tunakwama na tunawezaje kubadilika na kuwa bora.
🎙️ MWANAHISABATI Life lessons, ideas na conversations kuhusu maisha, mindset, psychology, money, discipline na kujijenga.
📚 Elimu bure. 💭 Think better. 🌱 Live better.
🎙️ Episodes mpya kila wiki.
//
MWANAHISABATI is a personal development brand exploring life as it really is—mindset, psychology, discipline, habits, money, philosophy, human behavior, and the things we experience while trying to build better lives.
I like to dig into ideas, research, books, and everyday life lessons, then break them down in a simple and relatable way. It’s not just about motivation; it’s about understanding why we do what we do, why we get stuck, and what we can do to change and become better.
🎙️ MWANAHISABATI Life lessons, ideas, and conversations about life, mindset, psychology, money, discipline, and personal growth.
📚 Free education. 💭 Think better. 🌱 Live better.
🎙️ New episodes every week.
I AM HIM MWANAHISABATI Arthur Geil
Connect with me:
X(Twitter): MWANAHISABATI @ArthurGeil
Website: mwanahisabati.com
Email: [email protected]