Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
MATENDO 2: 4
Katika uamsho Kanisa linapewa hakikisho kuu juu ya ukweli. Hiyo ndiyo jambo ambalo linatokea wazi katika Matendo ya mitume. Chunguza mitume hawa. Wiki chache kabla na baada ya Yesu kusulubiwa, walitetemeka sana na kukosa uhakika. Walikuwa wamemwamini Bwana Yesu Kristo, na kumjua kama Masihi. Lakini aliposulibiwa, wao walivunjika na kuchanganyikiwa katika akili zao.
Utapata, katika sura ya mwisho ya Injili ya Yohana, walipokuwa wakiongea ghafla Petero alisema, "Nitaenda kuvua samaki" .
Wengine walisema, "Tutakwenda pamoja nawe." Picha hii ni ya kufadhaisha zaidi. Walitikiswa na kukosa uhakika juu ya kila kitu. Bwana akawatokea, na kuwafundisha kisha uhakika huu ukawaweka katika hali bora.
Lakini ilikuwa tu baada ya kile kilichowapata kwenye Siku ya Pentekoste ndipo walijazwa na uhakikisho na uelewa. Mara wakaanza kuongea na watu juu ya kazi za ajabu za Mungu. Mashaka na ugumu wowote juu ya kuelewa ukayeyuka. Ndipo Petro akatoa mahubiri ambayo alihubiri katika tukio hilo. Alikuwa hakika kabisa mwenye uhakikisho. Hiyo ni kitu ambayo hutokea ulimwenguni kote wakati wa uamsho.