Mojawapo ya mahitaji muhimu ya mwili ni chakula na maji. Wagonjwa hupoteza hamu ya kula hata kunywa. Waliokufa hawana haja kabisa ya kula na kunywa. Yesu alitumia shauku hiyo ya njaa na kiu ya mwili katika kuisaka haki ya Mungu kiroho. Je, tunahisi njaa na kiu ya haki kiroho sawa na tuavyohisi njaa na kiu kimwili? La sivyo ama tunaumwa au tumekufa kiroho!