ONGEA ni Kijiwe rafiki kwa vijana, wa kike na wa kiume, wanafunzi na wazazi pia. ONGEA ni tamthilia ya redio inayohusisha maisha ya vijana (katika uhusika tofauti tofauti) wenye Umri wa rika balehe kati ya miaka 15-19 Pamoja na Wazazi/walezi wao. Vipindi hivi vya Ongea vimeandaliwa na Tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) na Tume ya kudhibiti ukimwi Zanzibar (ZAC) kwa kushirikiana na UNICEF, pamoja na wadau wengine. Kipindi cha ONGEA Kinawafikishia vijana taarifa sahihi, Ujumbe sahihi kuhusu VVU/UKIMWI, Afya ya Uzazi, Lishe bora, Stadi za Maisha , Usafi wa Hedhi na Mimba za utotoni.