Damu Azizi ya Kristo si alama tu ya mateso yake, bali ni chemchemi ya ukombozi, upatanisho na heshima mpya kwa kila mwanadamu.
Katika kipindi hiki, Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu – Sauti ya Faraja, anafafanua kwa kina uhusiano kati ya Damu Azizi ya Kristo na hadhi ya mwanadamu kwa mwanga wa imani ya Kikristo.