Yesaya Software Podcast

Safari ya Naamini kwenye Android Apps Development


Listen Later

Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Naamini Yonazi yeye ni Android Developer, pia ameshiriki kwenye makongamano ya Developer mbalimbali kama msemaji (ndani na nje ya nchi) vilevile ameandaa meetup kadhaa za Developers. Nilipenda fahamu safari yake na kufika alipo na je alipitia njia gani?

Naamini amenieleza alikuwa na kampani nzuri akiwa chuo ambayo ilimsaidia kufanya mazoezi zaidi kwenye programminng. Pia jamii ya Developer (mfano @gdgdar) ni chachu ya yeye kupanua uelewa na mahusiano baina na Developers. 

Amenieleza kuhusu changamoto alizokabiliana nazo wakati akianza kazi, kubwa ikiwa na kutopata sauti ya kusikika hasa kwa developer wakike. Kutokuaminika kama wanaweza fanya code kama vijana wakiume. 

Amenieleza hali imekuwa ikiimarika na hivyo hata kwenye ajira kwa wadada kama uko vizuri fursa ni nyingi na unachotakiwa ni kuonyesha uwezo wako katika kazi. 

Kwa haya na mengine mengi unaweza fuatilia toleo hili nilipozungumza na Naamini Yonazi.

...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Yesaya Software PodcastBy Yesaya R. Athuman

  • 5
  • 5
  • 5
  • 5
  • 5

5

2 ratings