Hey, Mambo vipi,
Leo tutazungumza kuhusu kugoogle au kutafuta majibu ya changamoto unapokuwa kwenye ujenzi wa mfumo. Je, unajisikia vibaya unapogoogle mambo kwenye mtandao kama programmer unanielewa nikisema Stack Overflow. Lakini je, kugoogle kunakufanya wewe kuwa programmer mbaya?
Nitakueleza kwa uzoefu wangu pamoja na programmers mashuhuri kabisa ninaowafahamu ambao pia wameshare uzoefu wao katika hili. Nitakueleza pia kuna time unagoogle na hutapata kitu lakini kuna mtu unamjua ana uzoefu na sala unalohaingaika nalo, nakumbuka usemi wa waswahili, KUULIZA sio Ujinga.
Hii ni Yesaya Software Podcast episode namba 34.